Spika afanya ziara katika Moja ya Hospitali zinazotaka kuwekeza nchini!!

Spika wa Bunge Mhe. Samuel Sitta akionyeshwa moja ya Vitanda bora na vya kisasa na Daktari mkuu Professor Yaman Tekant katika hospitali ya ACIBADEM Nchini Uturuki mara baada ya kutembelea hospitali hiyo jana. Hospitali hiyo inamilikiwa na makampuni binafsi ya ACIBADEM Health Group ambayo yameonyesha nia ya kuja kufanya utafiti nchini Tanzania kwa ajiri ya kuwekeza katika sekta ya afya. Katikati ni Mhe. Suzani Lyimo Mbunge wa Viti Maalum (Chadema) . (Picha zote na Owen Mwandumbya)
Spika wa Bunge Mhe. Samuel Sitta akitembela hospitali ya ACIBADEM Nchini Uturuki katika ziara aliyoifanya kujionea Teknolojia mbalimbali katika sekta ya Afya nchini humo. Kushoto ni Daktari mkuu wa Hospitali hiyo Professor Yaman Tekant na kulia ni daktari bingwa wa Kansa prof. Dr. ENIS OZYAR ambaye pia alishawahi kufanya kazi katika hospitali ya Ocean Road nchini Tanzania . Hospitali hiyo inamilikiwa na makampuni binafsi ya ACIBADEM Health Group ambayo yameonyesha nia ya kuja kufanya utafiti nchini Tanzania kwa ajiri ya kuwekeza katika sekta ya afya.
Spika wa Bunge Mhe. Samuel Sitta akionyweshwa moja ya mitambo ya kisasa ya kutibu kansa kwa njia ya mionzi na Daktari mkuu Professor Yaman Tekant katika hospitali ya ACIBADEM Nchini Uturuki mara baada ya kutembelea hospitali hiyo jana. Hospitali hiyo inamilikiwa na makampuni binafsi ya ACIBADEM Health Group ambayo yameonyesha nia ya kuja kufanya utafiti nchini Tanzania kwa ajiri ya kuwekeza katika sekta ya afya.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment