Kocha wa timu ya Simba Patrick Phiri kulia akiwa na mchezaji wake Juma Jabu pamoja na meneja wa timu hiyo Inocent Njovu katikati wakijiandaa kupanda ndege kuelekea Kigali Rwanda hivi karibuni.
Hatimaye mshambuliaji wa timu ya Simba Mussa Hassan Mgosi ameipaisha timu yake baada ya kufunga goli kwa njia ya penati katika dakika ya 90 ya mchezo uliochezwa nchini Rwanda katika michuano ya kombe la klabu bingwa Afrika Mashariki na kati baada ya timu hiyoya Simba kuibanjua timu ya Atraco goli 2-1 mchezo uliomalizika jioni hii.
Goli la kwanza la Simba lilifungwa na mshabuliaji mpya wa timu hiyo mganda Robert Ssentongo aliyesajiriwa kutoka timu ya Azam FC ya jijini Dar es salaam,
Timu ya Atraco ilijipatia goli la kufutia machozi dakika ya 76 ya mchezo huo hivyo mpaka mwisho wa mchezo huo matokeo yalikuwa Simba ya Tanzania 2 na Atraco ya Burundi 1 hivyo Simba imejitengenezea mazingira mazuri ya kusonga mbele katika kundi lao kwenye michuano hiyo.
1 comments:
Tupe na matokeo ya Simba na Sofapaka.
Post a Comment