Benjamin Sawe-Maelezo
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la makazi katika shirika la umoja wa mataifa Anna Tibaijuka amesema ili Afrika iendelee ni lazima kuwe na ujenzi wa makazi salama ikiwa ni pamoja kuwaendeleza kina mama na watoto..
Mkurugenzi Tibaijuka alisema kwa hivi sasa Tanzania imepiga hatua katika kuwaendeleza kinamama na kusema kuwa juhudi zaidi zinatakiwa katika kujengea uwezo rasilimali watu ili kuliletea maendeleo taifa.
Pia alisema tatizo la miundombinu likirekebishwa litawavutia kwa kasi wawekezaji kuja kuwekeza katika bara la Afrika kwa kuamini kuwa mitaji yao itakuwa sehemu salama.
Alisema Afrika imejaliwa na rasilimali nyingi hivyo ni wakati muafaka kwa waafrika kuamka na kutumia rasilimali zetu ipasavyo kwa maendeleo ya waafrika na si kwa watu wa mataifa mengine pekee.
"Afrika tumejaliwa na rasilimali nyingi ambazo mataifa mengine hawana hivyo ni muhimu kuzitumia rasilimali zetu ipasavyo ili tufaidike nazo na si kuwanufaisha mataifa mengine".
Alisema bila ya kutatua changamoto ya ujenzi wa makazi holela,uharibifu wa miundombinu,uwezeshaji wa rasilimali watu ikiwa ni pamoja na uboreshaji wa sekta ya Afya Bara la Afrika halitapiga hatua kimaendeleo.
Mkurugenzi Tibaijuka alisema matarajio yake katika mkutano unaoendelea hivi sasa wa hali ya uchumi duniani na hasa nchi za Afrika ni kushirikiana na mataifa mbalimbali katika kuboresha changamoto zinazoikabili Afrika ili iweze kupiga hatua katika maendeleo.

0 comments:
Post a Comment