Mbatia asema Nccr Mageuzi inaunga mkono mgomo wa wafanyakazi!!


MWENYEKITI wa Chama Cha NCCR Mageuzi James Mbatia ameunga mkono mgomo wa wafanyakazi na kuwataka wafanyakazi kuepuka kudanganyika na pipi (hoja za kisiasa).

Mbatia alitoa hoja hiyo jana jijini Dar es Salaam alipokuwa akifungua kikao cha Halmashauri kuu Taifa ya Chama hicho.“Mgomo wa wafanyakazi tunauunga mkono mia kwa mia, wanahaki kabisa ya kudai haki zao, kinachotakiwa ni wao kuwa na umoja ili waweze kujadili mambo yao ya msingi pamoja na kuepuka utofauti kati yao.
“Serikali inatakiwa kujifunza zaidi katika sherehe za mwaka huu, tena inatambua kuwa mgomo huo utakapotimia nchi itarudi nyuma kiuchumi kwa asilimia kubwa kutokana na athari zinazoweza kutokea,” alisema.
Aidha Mbatia alimtaka Rais kuwashirikisha wanauchumi na wanasheria katika suala kutatua matatizo ya wafanyakazi ili kuweza kusaidia kupata ufumbuzi wa kudumu wa matatizo hayo.
Kulia katika picha ni Katibu Mkuu wa Chama cha NCCR Mageuzi Samwel Ruhuza kulia na kushoto ni Makamu kutoka Zazibar Haji Ambasy Khamis

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment