Matukio katika picha mkutano wa ADB mjini Abidjan!!

Mkurugenzi wa Uwekezaji na Maendeleo ya Sekta Binafsi wa Soko la Pamoja la Mashariki na Kusini mwa Afrika (COMESA) Dkt Chungu Mwila akielezea leo kwenye mkutano 45 wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) jinsi mpango wa ruzuku ya mbolea kwa wakulima nchini Tanzania ulivyowasaidia wakulima kuongeza uzalishaji wa mazao mbalimbali. Wengine ni Mrugenzi wa Idara ya Kilimo wa ADB Aly Abou-Sabaa(kushoto) na Afisa Sera wa Shirika linalojulikana kama Alliance for a Green Revolution in Africa lenye makao yake nchini Kenya Dkt Augustine Langyintuo(kulia)
(Picha na Tiganya Vincent, Abidjan)
Kamishna Idara ya Fedha za Nje wa Wizara ya Fedha na Uchumi ya Tanzania Ngosha Magonya akichangia mada leo mjini Abidajan nchini Ivory Coast juu ya nchi za Afrika zinavyoweza kusaidia kuchangia ruzuku ya mbolea kwa wakulima kwa ajili ya kuleta mafanikio katika sekta ya kilimo.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment