MAHAKAMA YA KISUTU YAPIGA STOP UCHAGUZI SIMBA!!

Mahakama ya hakimu Mkazi KISUTU jijini DSM imesitisha uchaguzi wa klabu ya soka ya SIMBA leo ambao ulipangwa kufanyika keshokutwa ,MEI 9 mwaka huu hadi kesi ya msingi iliyofunguliwa na mmoja wa wanachama wa klabu ya SIMBA, MICHAEL WAMBURA mahakamani hapo itakaposikilizwa na kutolewa maamuzi mwishoni mwa mwezi huu.

WAMBURA alipinga uchaguzi huo kwa madai kuwa haujafuata katiba ya klabu hiyo na amenyimwa haki yake na TFF kwa sababu ambazo anataka TFF izithibitishe dhidi yake mbele ya mahakama.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment