Dennis Obua afariki dunia!!

Dennis Obua

Mwanasoka maarufu katika kanda ya Afrika Mashriki Dennis Obua amefariki dunia.

Obua aliwahi kushikilia wadhifa mbalimbali wa soka kama vile Rais wa CECAFA na mkuu wa chama cha soka Uganda –FUFA, na pia alikuwa mchezaji nyota wa zamani wa timu ya taifa ya Uganda, The Cranes.

Obua siku ya Jumanne asubuhi katika uwanja wa mpira wa Nakivubo wakati wachezaji wa zamani wakifanya mazoezi kwa mechi ya siku ya Jumatano kesho dhidi ya wabuge wa
Uganda, kusaidia waathiriwa wa maporomoko ya udongo yaliyotokea mwezi wa Machi mashariki mwa Uganda.

Taarifa zaidi zinasema Marehemu Obua alikuwa akilalamika maumivu ya kifua na baadae akaanguka. Gari la kubeba wagonjwa liliitwa na akapelekwa katika hospitali ya BAI Old Kampala ambapo alitangazwa amekufa.

Marehemu Dennis Obua mwanawe David Obua, ni mmoja wa wachezaji wa timu ya taifa ya Uganda, the Cranes ambaye anacheza soka katika klabu ya Hearts ya Scotland. http://www.bbcswahili.com/

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment