BREAKING NEWZZZZZZZZZZZZZZ! TUCTA WASALIMU AMRI NA KUSITISHA MGOMO!!

Rais wa Shirikisho la Vyama vya wafanyakazi TUCTA Ayubu Omary kushoto amezungumza na vyombo vya habari leo na kueleza nia yao ya kusitisha mgomo uliokuwa uanze kesho nchini kote, akizungumza katika ukumbi wa shirika la kazi la Umoja wa Mataifa ILO amesema wanamuamini Mh Rais Jakaya Kikwete na wanaamini kuwa matatizo yao yanaweza kutatuliwa

Hivyo akasema mgomo huo umesitishwa hautakuwepo tena mpaka watakapokutana tarehe 8 Mei kwa majadiliano zaidi na wanaamini kuwa masuala ya mishahara na kodi zinaokatwa kwa wafanyakazi vinaweza kupatiwa ufumbuzi katika kikao hicho.
PICHA NA MWANAKOMBO JUMAA WA MAELEZO.

Hapa akionyesha nyaraka mbalimbali ambazo zinazohusu mawasiliano ya TUCTA na Serikali

Hapa wakiimba wimbo wa mshikamano wa wafanayakazi kabla ya mkutano huo kufanyika.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment