Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger amesema timu yake "isahau mbio za kuelekea ubingwa" baada ya kufungwa mabao 2-1 na watani wao wa jadi Tottenham.
Gunners wako pointi sita nyuma ya vinara wa ligi kuu ya England Chelsea wakiwa wamesaliwa na michezo minne.
Gunners wako pointi sita nyuma ya vinara wa ligi kuu ya England Chelsea wakiwa wamesaliwa na michezo minne.
Wenger amesema "Ni lazima tusahau kuwania ubingwa na tujaribu kumaliza nafasi za juu kadri itakavyowezekana. "Bahati haikuwa upande wetu lakini hata hivyo lolote linawezekana."
"Inaonesha hatujakomaa vya kutosha kwa sababu huwezi kupoteza michezo kama hii iwapo unakusudia kushinda ligi."
"Inaonesha hatujakomaa vya kutosha kwa sababu huwezi kupoteza michezo kama hii iwapo unakusudia kushinda ligi."
Arsenal katika michezo minane iliyopita haikufungwa na kuweza kujizolea pointi 22 kati ya 24 ambazo ingeweza kuzipata, hatua iliyowaweka katika nafasi nzuri ya kushinda taji la ubingwa wa Ligi Kuu ya England kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2004.
Gunners msimu huu ilmekumbwa na tatizo la wachezaji wengi muhimu kuumia akiwemo Robin van Persie, Cesc Fabregas, Andrey Arshavin, William Gallas, Johan Djourou, Alex Song, Aaron Ramsey na Kieran Gibbs, wote wamekosa kucheza michezo muhimu kwa baadhi ya wakati.
Wenger ameongeza"Tumepiga hatua kubwa msimu huu lakini usiku huu wachezaji wengi muhimu hawakucheza." Katika mchezo huo Wenger alimchezesha Van Persie akiwa mchezaji wa akiba.
Wenger ameongeza"Tumepiga hatua kubwa msimu huu lakini usiku huu wachezaji wengi muhimu hawakucheza." Katika mchezo huo Wenger alimchezesha Van Persie akiwa mchezaji wa akiba.
0 comments:
Post a Comment