Leo ndani ya www. fullshangwe.blogspot.com kingkif wa www.kingkif.com
nakuja na jambo moja la musingi sana kwa wasanii wetu wa muziki.Hapa
haijalishi ni muziki upi?! Maana yangu ni Bongo Flava , Taarab ,
Muziki wa Dansi na Bongo Hip-Hop.
Kwakuwa mimi ni mdau mkubwa wa anga hizi kwa zaidi ya mikaka kumi na
tano sasa! Nimebahatika kuwa jirani mno na wasanii wa anga hizi.Katika
ujirani wangu huo na wao , nimegundua wasanii na wanamuziki wengi ni
wavuta bangi walipindukia kama !
Asilimia kubwa ya wasanii na wanamuziki wanatumia bangi kwa sababu zao
binafsi na hii nimeweza kufahamu baada ya kuwa nawaonya huku
nikiwahoji ni kwanini wameamua kuvuta bangi tena labda mbele yangu?!
Kwa kuwa kuna waliowahi kuvuta bangi huku na mimi nikiwepo jirani na
baada ya dakika kadhaa huwenda kupanda jukwaani na kuanza kushughulika
, huwa nawaona na kugundua uwezo wao unaathirika sana.
Lakini jambo la ajabu ni kwamba , katika majibu yao kwa ujumla eti
huwa wanasema wanapovuta bangi kabla ya kupanda jukwaani huwa wanapata
ujasiri wa hali ya juu sana!!!
Kuna mmoja anaimba kwenye bendi fulani hivi huwa ni rafiki yangu
mpendwa , basi bwana wiki iliyopita nilimkuta analiwasha alinijibi
hivi :
"King Kif acha mambo yako kabisa , unajua huu muziki hukunifundisha
wewe japokuwa wewe ni rafiki yangu lakini umenikuta nikiwa juu kwenye
gemu, sasa haya mambo yako eti ya kunishauri kuacha bangi mimi naona
utakwama tu. Mbona kuna vitu vingi huwa unaniambia na nakuelewa mara
moja tu , hili umekwama tena nakumba usije ukaniambia tena.Wewe ujui
kwamba mara baada ya kuliwasha huwa nafanya vitu bab' kubwa pale
jukwaani?Huwa nipo full uhakika , kuna mambo nayafanya pale ni magumu
mno ila wewe na watazamaji wengine huwa hamjui halafu mnajifanya
kufurahi tu!
Mtu mzima nilichoka kisha nikazima zangu!!! Nikaacha bangi ipo mkononi pake
mimi nikasepa chobingo fulani hivi kucheki mishemishe nyingine.
Sasa , kichwani nikabaki nawaza kuhusu majibu haya , kwamba eti
wakivuta bangi kuna ujasiri unaongezeka pele jukwaani! Mbona mimi
naona uwezo wao wa kupafomu unashuka! Inakuwaje wanapokuwa na bangi
kichwani eti wanajiona mashujaa ?! Hivi ni kweli uwezo wao unapanda
ama unashuka?
Haya, kuna mmoja yeye anamiliki bendi mpya ya muziki wa dansi na kwa
wakati huu huwa inatumbuiza mara mbili kwa wiki, yeye katika majibu
yake dhidi ya maswali yangu alijibu hivi:
"Unajua rafiki yangu King Kif bangi huwa inanifanya kuona kila jambo
ama kila kitu pale stejini kipo bomba tu , kuna kipindi wanamuziki
wangu huwa naona kama vile wanakosea lakini mimi mzuka huwa
umeishapana kichwani basi napuuzia tu na mambo yanaendelea.Sasa kama
ningekuwa sijavuta siningewagombeza na ningearibu kazi?!
Haya jamani hii makala nimeifanyia utafiti na wasanii na wanamuziki
wetu wengi ni wavuta bangi .Lakini binafsi sijachoka na sasa namtafuta
dokta mmoja ili anape maelezo yakutosha ya athari za bangi ili nikiaa
na wasanii na wanamuziki wetu niweze kuwaeleza kiunagaubaga .Ni mimi
Sigfred Peter Kimasa kutoka www.kingkif.blospot.com.

0 comments:
Post a Comment