Uhuru wa Kuongea Jmartins apagawisha mashabiki Dar!!.

Jamaa alinogewa na ushabiki wa bongo akaona bora avue koti na kofia ili kupagawisha wabongo,kila mtu aliondoka meno yote nje baada ya J-martins kufunga Usiku wa uhuru wa kuongea na kibao chake Good Or Bad,pichani J-martins akiimba kwa hisia kwa kweli ulikuwa ni usiku wa Uhuru wa Kuongea.
Hivi ni kwanini kila msanii anayetoka nje ya Tanzania ni lazima aombe kucheza na wasichana wa Kibongo jukwaani hii inamaanisha nini?na dada zetu wanapagawa kweli wakiitwa kwenye jukwaa kama inavyoonekana pichani J-martins akicheza na flowers wabongo.

Mashabiki wa J-martins meno 30 yote yalikuwa nje baada ya kumuona mwanamuziki huyo jukwaani akifanya mambo makuwa kama unavyowaona mashabiki wakifurahia onesho hilo

Onesho hili lilivuta hisia za mashabiki wengi kama picha hii inavyoonyesha mashabiki wakiangalia jukwaani kwa hisia wakati mwanamuziki huyo alipokuwa akiimba hata hivyo tathmini inaonyesha wanawake walikuwa ni wengi kuliko wanaume,pichani mashabiki wakifurahi wimbo wa mwisho uliofunga Usiku huo.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment