TIMU YA TAIFA YA POOLTABLE YAELEKEA UGANDA KESHO!!

Meneja wa bia ya Safari Lager Fimbo Butala akiongea na waandishi wa habari jijini juu ya safari ya timu ya taifa ya Polltable kulia ni katibu mkuuu wa chama cha Polltable Bw.Amos Kafwinga.


Timu ya taifa ya Polltable inatarajiwa kuondoka kesho kwenda nchini Uganda kwa ajili ya michezo kadhaa ya kirafiki katika kujiandaa na mashindano ya dunia yanayotarajiwa kufanyika nchini Ufaransa Novemba mwaka huu ambapo timu hiyo ni moja ya timu itakayoshiriki katika michezo ya dunia.

Akizungumzia safari hiyo katika mkutano na waandishi wa habari Meneja wa kinywaji cha Safari Lager Fimbo Butala amesema kampuni ya TBL kupitia bia yake ya safari Lager imeamua kudhamini timu hiyo kwa maandalizi ya safari kwa ajili ya michezo ya kirafiki.

Timu hiyo inaondoka kesho na wachezaji 10 wanane wakiwa wanaume na 2 wakiwa wanawake na watakuwa na michezo Kampala na Entebe kuanzia tarehe 23 mpka 26 aprili huku wakicheza kwa kutumia sheria za 1-2-3.

Timu hiyo pia inaondoka na Viongozi 4 na mwalimu, mara baada ya kurejea nchini kutafanyika utaratibu wa kuandaa safari nyingine kwa timu hiyo ya Taifa ya Pooltable kwenda kucheza michezo mingine ya kirafiki katika nchi za Kenya Zambia na Malawi, TBL inaidhamini timu hiyo kwa shilingi milioni 5 za kitanzania kwa ajili ya kufanikisha safari hiyo malazi pamoja na chakula.
Timu ya Taifa ya Pooltable ni ya tano kwa viwango vya ubora katika nchi 14 za afrika zinazotambuliwa na shirikisho la mchezo huo la Afrika.irafiki nchini Uganda katika dhana ileile ya kukuza michezo nchini.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment