Kamati hiyo ya mashindano pia imewaondoa Zakaria Haspope aliyekuwa akigombea nafasi ya Mwenyekiti pia kwa kuwa yeye aliwahi kuhukumiwa kwa kosa la uhaini na kutoka katika kifungo kwa msamaha wa rais.
Aden Rage ambaye pia alikatiwa rufaa yeye kamati hiyo imemuona hana hatia na anafaa kuendelea kugombea kwakuwa ana sifa za kugombea pamoja na kwamba aliwahi kushitakiwa katika mahaka na kutiwa hatiani lakini alikata rufaa mahakama ya rufaa na mahakama hiyo kumsafisha na tuhuma hizo.
Kamati ya uchaguzi pia imemwondoa katika kinyaganYiro hicho Chano Almasi aliyekuwa akigombea ujumbe wa kamati ya utendaji kwa kutotimiza majukumu yake wakati alipokuwa kiongozi katika klabu hiyo lakini pia majina yake yameonekana kuwa na mkanganyiko.
aliyekuwa katibu mkuu Mwina Kaduguda pia ameondolewa kugombea nafasi ya makamu Mwenyekiti kwa kuwa naye alishindwa kutimiza majukumu yake wakati alipokuwa katibu mkuu wa klabu hiyo katika uongozi unaomaliza muda wake.
Hivyo kinyang'anyiro kwa upande wa mwenyekiti kinabaki kwa Hassan Hasanoo,Andrew Tupa na Aden Rage wakati kwa upande wa makamu Mwenyekiti amebaki Godfrey Nyange Kaburu peke yake.
0 comments:
Post a Comment