RAINFRED MASAKO WA ITV KUMVAA JUMA NGASONGWA ULANGA MAGHARIBI!!

Mtangazaji na mwandaaji wa vipindi wa siku nyingi ITV na Radio One Rainfred John Masako akizungumza na waandishi wa habari leo kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo wakati alipotangaza nia yake ya kugombea ubunge katika jimbo la Ulanga Magharibi kupitia chama cha Mapinduzi CCM katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu hapa nchini, Mbunge wa sasa wa jimbo hilo ni Juma Ngasongwa aliyewahi kuwa Waziri serikalini katika vipindi Tofauti.
Rainfred Masako aliyezaliwa mwaka 1952 katika Wilaya ya Ulanga amesema muda alioitumikia jamii katika masuala mbalimbali unatosha sasa anataka awasaidie wananchi wa Jimbo la Ulanga kupitia Siasa, akaongeza kuwa yeye ni dhahabu iliyokuwa ikitembea na sasa ili wakazi wa jimbo la Ulanga waichimbe na kuipata ni kumpa ubunge yeye ili wasaidiane katika kuinua uchumi wa wakazi wa jimbo hilo, aliyeko kushoto katika picha ni Abdon Kidege mshauri wa Rainfred Masako masuala ya Siasa.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment