Misri mwenyeji wa mkutano wa vifaa kongwe!!


Maafisa wa utamaduni ulimwenguni wanatarajiwa kujadili namna ya kurejesha upya hazina ya sanaa zilizo kongwe ambazo wanasema ziliibwa na kutolewa katika maonyesho nje ya nchi.
Nchi 16 zitawakilishwa katika mkutano wa siku mbili mjini Cairo.
Imeandaliwa na baraza kuu la vifaa vya kale (SCA), linalotaka vifaa vingi vya mafarao virudishwe kutoka kwenye makumbusho ya nchi za magharibi.
SCA limesema mkutano huo utajadili ulinzi na fidia wa urithi wa utamaduni.
Wawakilishi ni pamoja na maafisa wa masuala ya utamaduni kutoka Ugiriki, Italia na China, wote ambao wamepoteza vifaa kongwe vyenye nakshi katika karne nyingi zilizopita ambapo sasa wanataka zirudishwe.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment