KOCHA WA TIMU YA YANGA KOSTADIN PAPIC ALIVYOISHANGILIA SIMBA!!

Kocha wa Yanga Mserbia Papic akiwa ameshikilia jezi ya Simba mara baada ya mashabiki wa Simba kumkabidhi jezi hiyo wakati alipokuwa amekaa kwenye jukwaa la Simba wakati wa Mchezo kati ya Timu ya Simba na timu ya Haras El-Hodood ya Misri katika michuano ya kombe la Shirikisho la CAF uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam jana ambapo Simba iliibuka na ushindi wa magoli 2 kwa 1.
Mshabiki wa Simba akimkabidhi jezi mchezaji mpya wa Simba abdulhumud Salim aliyetoka Mtibwa Sugar na kujiunga na timu hiyo.
Mdau wa Simba Nick Magarinza aka (Nick But) mwenye fulana nyekundu akiwa amepozi huku akifuatilia mchezo wa jana katika ya simba na Haras El-Hodood ya Misri,
Mussa Hassan Mgosi akiwatoka mabeki WAPINZANI wa Simba kwenye Kombe la Shirikisho Afrika, Haras El-Hodood ya Misri wakati wa mchezo wao uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa jana na simba kushinda magoli mawili kwa moja.

Benchi la ufundi la timu ya simba likiongozwa na kocha Mzambia Parick Phiri kushoto na Inocent Njovu meneja wa timu hiyo na kocha msaidizi Samri Said pamoja na wachezaji wa timu hiyo

Wachezaji wa Simba wakishangilia goli mara baada ya mgosi kufunga goli la pili

Emmanuel Okwi akifunga goli la kwanza la Simba wakati wa mechi yao dhidi ya waarabu wa Haras El-Hodood ya Misri.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment