HELLEN DAUSEN ATWAA TAJI LA MISS UNIVERSE TANZANIA 2010!!

Mkurugenzi wa kampuni ya Compass Communications na Mwandaaji wa Miss Universe Maria Sarungi kulia akimkabidhi maua mshindi wa shindano la Miss Universe Tanzania 2010 HELLEN DAUSEN baada ya kutwaa taji hilo katika shindano lililofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam, mrembo huyo atawakilisha nchi katika shindano la dunia la Miss Universe hapo baadae. Picha kwa hisani ya http://www.janejohn5.blogspot.com/
Miss Universe Tanzania katikati Helen Dausen akiwa na warembo wenzake walioshika nafasi ya tatu na ya pili.
Warembo walioingia tano bora wakiwa katika picha ya pamoja.
Kikundi kikitoa Burudani wakati wa shindano hilo.
Vazi la ubunifu.
Warembo walioshiriki kwenye shindano la Miss Universe wakiwa katika mavazi ya ubunifu wakati wa shindano lao lililofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam usiku wa kuamkia leo.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment