HALI YA UCHUMI DUNIANI SASA SHWARI!

Mshauri wa Uchumi wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na Mkurugenzi wa Idara ya Utafiti Bw. Olivier Blanchard akitoa ufafanuzi juzi washington DC kwa waandishi wa habari juu ya kuimarika kwa uchumi wa dunia.
Na Mwandishi maalum.
Mshauri wa Uchumi wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na Mkurugenzi wa Idara ya Utafiti Bw. Olivier Blanchard amesema kuwa uchumi wa dunia umerudi katika hali yake ya kawaida.

Bw. Blanchard alisema hayo juzi wakati wa mkutano na waandishi wa habari mjini Washington DC.

Alisema kuwa hivi sasa uchumi unatarajiwa kukua hadi kufikia asilimia 4.2 kwa mwaka 2010, ambapo utakuwa umepanda kwa asilimia 3 kutoka kwenye makadirio yetu ya mwezi Januari na kufikia asilimia 4.3 mwaka 2011.

Bw. Blanchard aliongeza kuwa mbali na ukuaji huo wa uchumi , biashara duniani imeiimarika na mitaji imeendelea kuongezeka.

Aidha aliendelea kueleza kuwa hali ya soko la fedha imeendelea kukua na kuimarika ambapo matokeo mazuri yameonekana katika nchi zilizoendelea na zinazoendelea .

Bw. Blanchard aliendelea kueleza kuwa wakiangalia kwenye nchi ambazo uchumi wao ni mkubwa zaidi wanakadiria uchumi unatarajiwa kukua kwa asilimia 2.3 kwa mwaka 2010, na asilimia 2.4 kwa mwaka 2011.

Alisema kuwa hali hiyo haitoshi kuziba pengo lililotokea katika kipindi cha mtikisiko wa uchumi duniani.

Aidha mchumi huyo aliendelea kuimarika kwa uchumi huu kunatufanya wajue changamoto ambazo zinawakabili ili wajipange upya katika kuimarisha uchumi dunia.

“Changamoto hizi hazikuja zenyewe, haikuwa kitu rahisi kabisa kufikia hapa tulipo, hivyo basi, nguvu ya ziada inahitajika kama vile kuwa na fedha za kutosha kwa nchi zilizoendelea , kuwe na marekebisho ya riba na uwiano wa mahitaji duniani kote.Hii ni kazi kubwa inayo wakabili watunga sera kwa miaka michache inayokuja” alisema Bw. Blanchard.


TAARIFA HII IMETOLEWA NA MSEMAJI MKUU
WIZARA YA FEDHA NA UCHUMI
WASHINGTON DC
21/04/2010

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment