Timu ya Chang’ombe Joging ya Temeke imefanikiwa kuibuka na ubingwa wa Mashujaa Sunday Soccer Bonanza baada ya kuibwaga timu ya Mabibo Veterani 1-0 mchezo uliochezwa katika uwanja wa Ukonga Magereza.
Jumla ya timu sita zilishiriki ikiwa ni pamoja na Mabibo Veterani,Kiwalani Veterani, Vingunguti Veterani, New Ukonga Veterani, Mtoni Veterani, na Chang’ombe.
Katika bonanza hilo Mgeni Rasmi alikuwa ni mwandishi na Matngazaji mwandamizi wa shirika la Utangazaji la Taifa TBC Elisha Elia ambaye alikabidhi zawadi ya Mbuzi kwa washindi.
Aidha mchezaji bora wa mashindano aliibuka Dallos Miwa wa Kiwalani ambaye alizawadiwa fulana zenye nembo ya Mashujaa Musica na Mfungaji bora wa mashindano alikuwa ni Abdallah Shomari wa Vingunguti ambaye pia alizawadia Fulana.
Katika bonanza hilo ambalo baadhi ya wageni walitoka sehemu mbalimbali akiwamo mwandishi na DJ wa kituo cha Radio cha Zanzibar- Bomba FM- DJ –Fax ambaye alifika kwa lengo la kufanya makubaliano ya kuishirikisha timu moja ya visiwani humo.
Kwa mujibu wa mratibu wa Bonanza Spia Mbwembwe, alisema kuwa timu zitakazoshiriki wiki ijayo ni pamoja na Savey Veterani, Kipunguni, Mashujaa Veterani ya Vingunguti, na timu ya Tabata Veterani.
Bonanza hilo linadhaminiwa na kampuni ya Mashujaa Group ambapo burudani kabambe kutoka Bendi ya Mashujaa Musica hutolewa live ikiwa ni katika kuwapa raha mashabiki wa soka.
0 comments:
Post a Comment