Askari waacha lindo na kukamata magari ni Benki ya NMB tawi la Bank House!!

Askari Polisi wa lindo Tawi la NMB Bank House jijini Dar es salaam wakiwa wameacha malindo yao jana (Ijumaa Kuu) na kukamata magari yanayokiuka sheria za barabarani (mtaa wa Samora). Hatua hiyo ni hatari kwani majambazi wanaweza kutumia mbinu hiyo ili kuwarubuni askari hao na kuvamia Benki kirahisi. Askari hao wamekuwa wakiendesha zoezi hilo wakati wa siku za mapumziko ya wiki (wikiendi) , Sikukuu na jioni.
Mmoja wa Askari wa lindo la Benki wa NMB Tawi Benki House akimkimbia mpiga picha baada ya kuona amefanya kosa la kuacha lindo na kuanza kukamata magari kama askari wa usalama barabarani jana jijini Dar es salaam.
Picha zote na Tiganya Vincent( Picha na MAELEZO)

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment