Mkurugenzi wa ASET Asha Baraka akizungumza na waandishi wa habari kwenye Klabu ya Much More leo wakati alipozungumzia Filamu mpya inayoitwa Lovely Gamble iliyotengenezwa na kampuni ya ASET kwa kumtumia muigizaji Kanumba na watanzania kadhaa.
Asha amesema filamu hiyo imetengenezwa nchini Uingereza kwa kumtumia mtoto wao anyesoma huko ambaye ameiongoza, kurekodi na kuiediti filamu nzima kwa kutumia kampuni yake ya Buzzie Production.
Kanumba ameshirikiana na watanzania wanaoishi nchini Uingereza, wakenya pamoja na wazimbabwe na lugha zilizotumika katika filamu hiyo ni kiingereza na kiswahili.
Ameongeza kwamba filamu hiyo itazinduliwa aprili 25 kwenye ukumbi wa Billicanas wakati wa onyesho la kawaida la bendi ya African Stars inayopiga kwenye ukumbi huo kila jumatano katikati ya wiki.
Amemaliza kwa kusema kama ilivyo kampuni ya ASET imeendelea kuthamini vipaji vya wasanii wa nyumbani na baada ya kutoa filamu ya "Tone la Damu" imeamua kutoka na filamu hii mpya ya "Lovely Gamble" ambayo mara baada tu ya kuzinduliwa itaanza kusambazwa na kampuni ya KAPICO LTD na itakuwa ikiuzwa kati ya shilingi 2000 kwa bei ya jumla.
0 comments:
Post a Comment