Portsmouth yapokonywa pointi tisa!


Klabu iliyo kwenye mzozo ya Portsmouth imepokonywa pointi tisa za Ligi Kuu ya England kutokana na kufilisika mwezi uliopita.
Hatua hiyo ina maana klabu hiyo inayoburura mkia katika msimamo wa Ligi Kuu ya England kwa sasa inachosubiri ni miujiza tu kuepuka kushuka daraja kutokana na michezo tisa iliyosalia.
Kabla ya kupokonywa ponti hizo Portsmouth ilifanikiwa kutia kibindoni pointi 19 na kwa maana hiyo wamesaliwa na pointi 10 tu hivi sasa.
Klabu hiyo inakabiliwa na deni la kiasi cha paundi milioni 65 na katika historia inakuwa klabu ya kwanza ya Premier League kufilisika.
Meneja wake Avram Grant alisema mwezi uliopita: "Soka ni lazima iamuliwe uwanjani na sio mahakamani au katika ofisi za Premier League."

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment