Moja ya boti za kijeshi za nchi za magharibi ikivinjari katika pwani ya bahari ya Hindi katika kulinda na kuzuia uvamizi wa maharamia hao katika meli.
Kenya imekataa kupokea washukiwa watatu wa kisomali ambao ni maharamia wanaoshikiliwa kwenye meli ya kivita ya Italia.
Kenya imesema magereza na mahakama zake hazina uwezo wa kuchukua kesi zaidi.
Mkuu wa polisi wa mjini Mombasa, Leo Nyongesa amesema amepokea maagizo kutoka serikalini kuwa asichukue washukiwa zaidi.
Kenya ni moja kati ya nchi mbili pekee zinazowapokea washukiwa wa uharamia wanaokamatwa na majeshi ya wanamaji ya nchi za magharibi.
Kenya imehukumu maharamia kumi na tisa na inawashikilia zaidi ya wengine mia moja. www.bbcswahili.com

0 comments:
Post a Comment