Uchimbaji mafuta Uganda wazua hofu.

Wasiwasi umeibuka kuhusu mipango ya makampuni ya mafuta ya Uingereza na Ireland kuchimba mafuta magharibi mwa Uganda.
Wanaharakati wa mazingira nchini Uingereza, wamesema kuwa serikali za Uganda na Uingereza, zimeruhusu kandarasi za uchimbaji wa mafuta ambazo zinafaidi makampuni hayo bila kujali maslahi ya wakaazi wa maeneo hayo wanaoishi katika umaskini.
Wanaharakati hao wa kikundi cha 'Platform' wanasema harakati za kutafuta mafuta nchini Uganda, huathiri mazingira.
Hata hivyo makampuni hayo ya kigeni yamesisitiza kuwa yatajitahidi kulinda mazingira na yanaunga mkono usimamizi bora wa sekta ya kibinafsi.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment