Timu ya Simba ya jijini Dar es salaam pamoja na kuwa na mchezo wa ligi kuu ya vodacom Tanzania leo kwenye uwanja wa uhuru kati yake na timu ya Africa Lyon, inatarajia kujitupa uwanjani tena jumamosi wiki hii ili kujipima na timu Zesco kutoka nchini Zambia.
Akizungumza na timu ya FULLSHANGWE afisa habari wa Simba Cliford Ndimbo amesema mchezo huo ni kwa ajili ya kujipima na kuangalia makosa katika kikosi cha Msimbazi kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa kimataifa ambao utafanyika katikati ya mwezi machi mwaka huu jijini Dar es salaam kuwania kombe la Shirikisho la CAF michuano ambayo timu hiyo inashiriki.
Ndimbo amesema timu ya Simba imejiweka sawasawa kimchezo na kocha wa timu hiyo Mzambia Patrick Phiri amekiandaa vizuri kikosi kwa ajili ya michezo yote ya Ligi kuu na ya kimataifa ili kiweze kukabiliana vyema na changamoto ya kimchezo kitakayokutana nayo kutoka kwa timu pinzani, na ni imani yetu kuwa kabla ya mchezo wetu wa kombe la shirikisho tutakuwa tumejiweka vizuri kwa mchezo huo.
Timu ya Simba inatarajia kucheza na timu ya Lengthens kutoka nchini Zimbabwe au As Adema ya Madagascar katika mchezo wake wa kombe la Shirikisho.
0 comments:
Post a Comment