Wafanyakazi wa huduma za wanyama pori nchini Kenya wameanza kuwakusanya maelfu ya pundamilia na wanyama wengine wanaokula majani na kuwapeleka katika hifadhi moja ambako simba wanaokabiliwa na njaa wanavamia mifugo.Ndege za Helikopta zinatumiwa kukusanya wanyama hao ambao baadae wanapakiwa katika malori na kusafirishwa hadi katika hifadhi hiyo.Lengo hasa ni kuongeza idadi ya wanyama hao katika hifadhi ya wanyama ya Amboseli ambayo imekabiliwa na upungufu wa wanyama hao uliosababishwa na ukame.Hali ambayo imesababisha simba na fisi kukosa chakula cha kutosha.Shughuli hii ya kuwahamisha wanyama hao ambayo itachukuwa mwezi mzima ndio kubwa zaidi kufanyika barani Afrika.
Maelfu ya Wanyama wahamishwa Kenya!!
Posted by
ADMIN
You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment