Tumedhibiti ghasia,asema mkuu wa jeshi Nigeria!

Wanajeshi wa Nigeria wakiwa na silaha zao wakati wa machafuko ya jimbo la Delta nchini humo.

Jeshi la Nigeria limesema limechukua udhibiti wa mji wa Jos,ambapo mapigano ya hivi karibuni kati ya waislamu na wakristo yalisababisha vifo vya watu kadhaa.
Luteni Kanali Shekari Galadima ameiambia BBC kuwa mji "uko shwari" wakati jeshi likihakikisha kuwa amri ya kutotoka nje kwa muda wa saa 24 inatekelezwa. Amesisitiza kuwa hakutakuwa na ghasia tena.
Lakini mwandishi wa BBC katika eneo hilo anasema ghasia sasa zimezidi hadi katika mji wa Pankshin, kilomita 100 kutoka Jos.
Makundi ya kutetea haki za binaadamu yanasema takriban watu 200 wanaaminika kufariki dunia tangu Jumapili.
Mji wa Jos umekumbwa na mapigano ya kidini kwa takriban muongo mmoja uliopita. http://www.bbcswahili.com/

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment