TANESCO MWOGOPENI MUNGU (ASKOFU ZAKARIA KAKOBE)!

Askofu Zakaria Kakobe kiongozi wa kanisa la Full Gosopel Assemblies Of God Tanzania lililopo Mwenge jijini Dar es salaam akizungumza mbele ya wanahabari wakati alipoongoza waumini wa kanisa lake kupinga kitendo cha shirika la umeme Tanzania (Tanesco) kuendelea na mradi wa kupitisha nyaya za umeme mkubwa katika eneo la kanisa lake kwa madai kuwa ni hatari kwa waumini watakapokuwa kanisani hapo askofu Zakaria Kakobe amesema hawataondoka kanisani hapo wataendelea kupiga kambi na kusali huku wakimlilia mungu mpaka kieleweke.
Waumini wa Kanisa la Full Gospel Ssemblies of God lililoko mwenge wakiwa wamepiga kambi katika kanisa hilo kuanzia leo kupinga kitendo cha Tanesco kuendelea na mradi wa kupitisha njia ya nyaya za umeme karibu na kanisa hilo kwa madai ya kuhatarisha maisha ya waumini wa kanisa hilo wakati wa kuabudu kanisani hapo wamesema hawako tayari kuondoka kanisani kwao mpaka Tanesco watakapoacha kufanya hivyo.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment