Wanamuziki wa bendi za African Stars na Fm Academia wanatarajia kupepetana katika mchezo wa mpira wa miguu januari 17/2010 katika bonanza linalofanyika kila jumapili kwenye viwanja vya Leaders jijini Dar es salaam.
Meneja wa bendi ya Fm Academia aliyefahamika kwa jini moja Mujibu amesema mchezo huo utafanyika kuanzia saa nane mchana kwa bendi hizo kucheza mpira wa miguu pambano ambalo litakuwa ni la kirafiki
Mujibu ameongeza kuwa lengo la mpambano huo ni kuwakutanisha wanamuziki wa bendi zote mbili lakini pia ni kujenga mahusiano mema kati ya wanamuziki wetu kwa kuwa muziki ni burudani na kila mtu anatakiwa kufurahia kazi yake ya muziki lakini pia ni wakati mzuri kwa wanamuziki wetu kubadilishana mawazo na mbinu za kimuziki.
Kama unavyoona katika picha hapa ni wanamuziki wa African Stars na FM Academia wakifanya mazoezi kwa pamoja kwenye viwanja hivyo vya Leaders kabla ya mchezo huo wa kesho wadau kaeni mkao wa kupashwa kwani mara baada ya mpambano huo kesho tutakuletea matokeo yake na mtajua nani ameibuka mshindi.
0 comments:
Post a Comment