Mapigano mapya Jos, Nigeria

Moja ya picha ikionyesha vurugu za mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yaliyowahi kutokea nchini Nigeria.

Ripoti kutoka nchini Nigeria zinasema kuwa mapigano makali yamezuka katika mji wa Jos, kati kati mwa nchi hiyo.
Watu saba wameripotiwa kufa na wengine wengi kujeruhiwa.
Mamia ya familia yametoroka makazi yao na sasa wanalala katika kambi za muda.
Mapigano hayo yalitokea katika wilaya ya Nassarawa Gwom, magharibi mwa mji wa Jos.
Mfanyakazi mmoja wa shirika la kutoa misaada ambaye alizungumza na BBC, amesema kuwa takriban watu 58 wamepelekwa hospitalini kwa matibabu, wengi wakiugua majeraha ya kukatwa katwa na panga.
Polisi wa kutuliza ghasia na wanajeshi wa Nigeria wanashika doria katika mitaa ya mji huo na wameweka agizo la kutotoka nje usiku kucha.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment