MANJU MSITA ALETA UBUNIFU MPYA KATIKA MAVAZI YA HARUSI!!

Emmanuel na Diana wakikata keki siku ya harusi yao huku matron wao akiwaangalia.
Hatimaye mbunifu wa mavazi Manju Msita amefanikiwa kubuni mavazi kwa ajili ya maharusi. mavazi yaliyovaliwa kwa mara ya kwanza na maharusi Emmanuel na Diana hivi karibuni harusi iliyokuwa ya kupendeza na ya kuvutia iliyofanyika hapa jijini Dar es salaam.
Mavazi hayo ni kwa ajili ya maharusi wote pamoja na wasimamizi wa pamoja na watoto wanaotangulia mbele kwa ajili ya kupamba harusi, Manju Msita mbunifu wa mavazi mwandamizi hapa nchini anayefanya kazi zake katika katika kituo cha sanaa cha Mikono House kilichopo makutano ya barabara za Nyerere na Chang'ombe amesema tayari wanandoa hao wameshatumia nguo zake kwenye harusi yao, ilikuwa ni harusi nzuri na walifurahia nguo hizo.
Manju anaendelea kueleza kwamba awali maharusi hao walikuwa na mashaka kama nguo hizo zingewapendeza kutokana na mazoea ya maharusi wengi hapa nchini ambao wamekuwa wakivaa suti na magauni marefu, nguo ambazo zimeshonwa kwa tamaduni za kimagharibi zaidi, anaongeza kuwa hata hivyo wanandoa hao walikubaliana na wazo lake na aliwatengenezea nguo nzuri ambazo walizitumia kwenye harusi yao,
Ilikuwa ni harusi ya kusisimua kwani watu wengi hawajazoea kuona maharusi wakiwa wamevaa nguo za maharusi zilizotengenezwa na kurembwa kwa tamaduni za kiafrika na kila mtu aliyewaona maharusi hao alitamani awaangalie mara mbili.
Anasema nguo hizo zinatengenezwa kwa kitambaa cheupe laini na kigumu huku kikichanganywa na rangi nyeusi kiasi huku nguo hizo zikinakshiwa na marembo yenye mchanganyiko wa shanga na baadhi ya vitambaa vigumu.
Manju anasema harusi hiyo imemuongezea neema kwani mpaka sasa ana tenda ya kushona nguo za harusi zipatazo 10 kwa muda mfupi tu, kitu ambacho hakikuwepo hapo awali kwani oda nyingi zilikuwa ni nguo za kawaida, haya ni mabadiliko yanayokuja kwa kasi sana katika sanaa ya ubunifu wa mavazi na huenda watu wasipendelee tena kuvaa suti kweye harusi hivyo nawakaribisha kuja kujipatia ubunifu huu mpya wa nguo za harusi watu wote wanaopenda kutukuza Uafrika wao.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment