MAKANISA YATAKIWA KUWAJALI WANAKWAYA WAO ILI WAWEZE KUDUMU KATIKA KWAYA HIZO!!

Producer Frank Kameta akiwa ofisini kwake.

Producer wa siku nyingi ambaye ameshawatoa wasanii kibao wa muziki wa bongofleva anayejulikana kama Frank Kameta hivi sasa ameugeukia muziki wa injili baada ya kutamba katika muziki wa bongofleva kwa muda mrefu.
Akizungumza na Mwana FULLSHANGWE. BLOG Kameta amesema ameamua kuinga katika muziki wa injili kwakuwa huko hakuna Ubabaishaji wa kimuziki, kwa maana ya waimbaji wa muziki wa injili wanajua muziki mana yake nini na hakuna kazi kubwa ya kusahihisha makosa yao katika uimbaji kama vile waimbaji wa muziki wa Bongofleva lakini pia malipo yao ya kazi hayana matatizo sababu kazi zao zinatoka.
Producer huyo maarufu nchini anasema ni kazi kubwa kufanya kazi na wasanii wa bongofleva hasa wale ambao hawajui hata kupiga gitaa au kinanda (Keyboard) kwani hata kanuni za muziki hawajui hivyo mnapoingia studio atajitahidi sana atarekodi nyimbo nzuri kwenye albam ya kwanza lakini baada ya hapo anashindwa kuleta ubunifu mpya kwenye albam inayofuata hali inayomfanya apotee katika gemu ya muziki.
Kameta anasema tayari amesharekodi albam za waimbaji wa injili wengi na wenye majina makubwa na albam zao zinafanya vizuri sana katika soko.
Amewataja waimbaji hao kuwa ni Ambwene ambaye amerekodi albam ya Matatizo ni radha, Bahati Bukuku na albam yake Nimesamehewa dhambi siyo Majaribu, Neema Mushi albam Raha jipe mwenyewe, Bonny Mwiteje na wengine wengi.
Lakini pia anasema tayari ameshamaliza kurekodi albam ya Ramadhan Masanja (Banza Stone) inayoitwa Photo yenye nyimbo nane huku akizitaja baadhi ya nyimbo ambazo ni Photo yenyewe,Mama Africa,Siri yangu na nyingine nyingi.
Anasema kutokana na kubadili mwelekeo wake wa kazi anashukuru kwani ameweza kujua mambo mengi katika muziki na pia si haba riski inapatikana vizuri na watoto wanakwenda shule, lakini pia amewataka viongozi wa makanisa na waumini kubadili mwelekeo. wawajali wanakwaya wao na kuwalipa angalau posho kidogo kutokana na huduma yao ya uimbaji .
kwani kwa sasa muziki wa injili ni biashara nzuri ambayo inanufaisha makanisa tu wakati wanakwaya pia wanakabiliwa na matatizo mengi ya kimaisha na ndiyo, maana waimbaji wengi wamekuwa wakikimbia na kuanza kuimba kwa kujitegemea kitu ambacho kimeonyesha kuwapa ahueni, na kutokana na hilo wanakwaya wengi sasa hivi wanakimbia kwaya zao na kuanzisha vikundi vyao vya uimbaji kwa kumalizia akawasihi wakuu hao kuliangalia hili ili wawasaidie hawa wanakwaya lakini pia jambo hili litawafanya wanakwaya kudumu katika kwaya zao na kutoa huduma vizuri zaidi makanisani


You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment