MADEREVA UBUNGO WAMTIMUA KATIBU MKUU WAKE!

Kituo cha Mabasi yaendayo Mikoani- UBUNGO
Umoja wa Madereva wa Mabasi Tanzania (UWAMATA) umemvua madaraka Katibu Mkuu wake Ndg Salum Abdallah kwa tuhuma za kuhujumu mipango ya Serikali kuhakikisha kuwa madereva wa mabsi wanapata mikataba ya ajira, mishahara na posho kwa mujibu wa sheria za ajira. Hii inafuatia kitendo cha Katibu Mkuu huyu kuficha habari kuhusu maamuzi ya Serikali kuhusu ajira za madereva wa mabasi.
Uamuzi wa kumvua madaraka Katibu Mkuu ulichukuliwa hivi karibuni na Baraza la Wadhamini la UWAMATA, baada ya wajumbe wanne kati ya sita, akiwemo Mwenyekiti wa Taifa wa UWAMATA kuunga mkono pendekezo hilo.
Kwa muda mrefu madereva wa mabasi wamekuwa wakiilalamikia Serikali kuhusu kutokuwa na mikataba, kutolipwa mishahara, posho na maslahi mengine kwa mujibu wa Sheria ya Ajira na Mahusinao Kazini namba 6 ya 2004, kiasi cha kufikia hatua ya kuitisha mgomo tarehe 14 Agosti 2009, na hivi karibuni kuitishwa kwa mgomo mwingine tarehe 09 Januari 2010, ambao ulifutwa dakika za mwisho.
Mwenyekiti wa Barza la Wadhamini la UWAMATA Ndg Chrizant Kibogoyo amesema kuwa kumvua madaraka Katibu Mkuu ni moja ya harakati za kuhakikisha kuwa unakuwepo uwajibikaji wa hali ya juu katika kuhakiksha kuwa ajali za barabarani zinapungua kwa madereva kupatiwa maslahi yao ili wasipate visingizio vya kuendesha kwa mwendo wa kasi.
Hivyo kitendo alichofanya Katibu Mkuu huyu cha kutofikisha maamuzi ya Serikali kwa wanachama, ambao ni madereva wa mabasi ni cha hujuma kubwa. Vitendo kama hivi ndivyo husababisha madereva kuichukia Serikali bure wakati ambapo viongozi kama hawa ndio hukwamisha jitihada za Serikali kutokana na maslahi binafsi wayapatayo kutoka kwa baadh ya wamiliki wa mabasi wasiotaka kulipa mishahara na maslahi mengine kwa wafanyakazi wao (Madereva)

Asante
Chrizant Kibogoyo

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment