Ameonyesha kuwa ni mwalimu anayejua kusoma mchezo na kuwapa mbinu wachezaji wake ili kuweza kumkabili adui wakati wote wa mchezo hivyo kuiweka timu katika mchezo mzuri na kujituma katika kufanikisha ushindi.
Mashindano haya ya kombe la Tusker yaliyomalizika ambayo timu ya Yanga ndiyo iliyoibuka mabingwa jana yameonyesha dhahiri uwezo wa kocha huyo baada ya kutopoteza hata mchezo mmoja, huku wachezaji wakicheza kwa kuelewana karibu michezo yote mpaka kufikia fainali na hatimaye jana ukafanikiwa kuitoa timu ngumu ya Sofapaka kutoka Kenya ambayo watu wengi walikuwa wakitabiri kuwa huenda ndiyo ingechukua ubingwa wa kombe la Tusker mwaka huu 2009 baada ya timu ya Simba kufungwa na kutolewa pia na Timu ya Yanga huku ikiambilia nafasi ya tatu baada ya kuifunga Tusker ya Kenya
Kinachotakiwa sasa ni kwa uongozi wa Yanga kumpa nafasi na ushirikiano kocha Papic ili aweze kufanya kazi yake ya kufundisha timu vizuri kama alivyoianza na hatimaye tuanze mzunguko wa pili wa Ligi kuu ya Vodacom kwa upinzani wa kweli wa kisoka uwanjani Hongera sana kocha PAPIC.
0 comments:
Post a Comment