MAADHIMISHO YA SHEREHE ZA MIAKA KUMI YA BONDE LA MTO NILE (NILE BASIN INITIATIVE)

Makamu wa Rais Dr. Ally Muhamed Shein akifungua rasmi mkutano wa siku tatu ambao unaambatana na sherehe za miaka kumi ya bonde la mto Nile (Nile Basin Initiative) mkutano huo unakutanisha Mawaziri wa maji na wajumbe mbalimbali kutoka nchi ambazo bonde la mto nile limepitia na utajadili mmambo mbalimbali kuhusu jinsi ya kulinda na kuhifadhi mazingira pamoja na changamoto zinazojitokeza juu ya uhifadhi wa bonde hilo na unafanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam (picha na mdau Bernad Rwebangira).
Makamu wa Rais Dk.Ali Mohamed Shein akiwa katika picha ya pamoja na mawaziri wa maji wa Bonde la Mto Nile mara leo baada ya kufungua mkutano wa siku tatu wa Nchi Shiriki za Bonde la Mto Nile (Nile Basin Initiative) ulioambatana na sherehe za kutimia miaka 10 tokea kuundwa kwa Ushirika huo, mkutano huo utajadili juu ya mafanikio yaliyopatikana tokea kuanzishwa kwake, changamoto pamoja na matarajio ya baadae katika kituo cha mikutano cha Mlimani City jijini.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment