![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhSvcfpfaX25WeDtP7zhG7tGuBKOp7KKX5YMzefvGmGjrmuXgaaakEZc_UfZtZjTOTN213zazdzj-ykkD7TZArLuVh3CNYDyKN2sLytQ5PL6iEEz85oD2nMsxK7XoUzZUJ8GQQE2Qh1fWP3/s400/mw.jpg)
Wamekamata mizoga 9 ya Tembo, 12 ya viboko ,16 ya Nyati, 2 ya kuro na mmoja wa mamba, pamoja na kuonekana kwa mizoga hiyo nyara zifuatazo zilikamatwa meno 8 na vipande 12 vya meno ya tembo vyenye uzito wa kilo 39, nyama ya Nyati na Swalapala, Ngozi moja ya Mbawala, na mkia mmoja wa nyumbu, pia kilo 20 za samaki wabichi.
Silaha zilizokamatwa ni Bunduki za kuwindia wanyama (RIFLE) 3 na ShotGun 15 , SMG 1, Magobole 2, risasi 114 kati ya risasi hizo 25 zimetengenezwa kienyeji, sumu aina ya Furudan itumikayo kuulia samaki, mamba hata viboko na kwa vile sumu hii huwekwa kwenye maji madhara yake yanampata pia binadamu anayetumia maji hayo.
Kwa maana hiyo basi Wizara itawashughulikia wahalifu ipasavyo vilevile itaendeleza doria za pamoja kati ya jeshi la polisi na idara ya wanyamapori, TANAPA,Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro(NCAA) na Taasisi nyingine za Kanda na Kimataifa katika kudhibiti Ujangili.
Operesheni imepewa jina la "Kipepeo" kutokana na kutumiwa kwa Helkopta na Ndege za kusafirisha askari katika vituo ndani ya pori ikiwa ni pamoja na kuhakikisha askari wanapatiwa mahitaji yote muhimu mahali popote walipo.
0 comments:
Post a Comment