Bendera ya Taifa yafika kileleni Kilimanjaro!!

Elly Gerald Minja
BENDERA ya Taifa iliyokimbizwa kwa miguu na wanariadha nyota kwa sikutano mfululizo, hatimaye jana ilifika kileleni mwa mlima mrefu kulikoyote barani Afrika, Mlima Kilimanjaro na kusimikwa rasmi kwenye kilelecha Uhuru kilichopo umbali wa futi 5895 kutoka usawa wa bahari.Mwanamichezo mwenye uzoefu wa aina yake katika kuupanda mlima huo,Elly Gerald Minja ndiye aliyeifikisha bendera hiyo mapema janaasubuhi.
Mbali ya Minja mkazi wa mkoani Kilimanjaro, wanariadha mashujaawalioandika historia ya kuzindua mbio hizo za aina yake nchiniwalikimbiza bendera huku wakipokezana kila baada ya kilomita kati ya10 na 15 kutoka Dar es Salaam hadi Marangu, Moshi mkoani Kilimanjarotangu Jumapili iliyopita.Zaidi ya wanariadha 70 nchini, wengi wakiwa wa kimataifa walikimbizabendera hiyo kwa zaidi ya kilomita 567. Walifika Marangu Alhamisijioni na siku iliyofuata baadhi yao walianza kuipandisha MlimaKilimanjaro bendera hiyo ambayo mbio zake zimeasisiwa na kudhaminiwana Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia Bia yake ya Kilimanjaro.
Nyota kama Francis Naali na binti yake, Mary Naali aliyeipa Tanzaniamedali ya shaba katika michezo ya Olimpiki iliyofanyika Beijing,China, Samwel Mwera, Sarah Maja walikuwa kivutio kikubwa kamailivyokuwa kwa Peter Pallagyo, mkongwe mwenye umri wa miaka 50 namalemavu wa mikono aliyewaikilisha nchi katika michuano ya Olimpiki naJumuiya ya Madola, Joro Mathias.Akiwa mwenye furaha isiyo kifani mara baada ya wanariadha kufikaMarangu, Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, George Kavishe alisemaamefurahishwa na jinsi Watanzania walivyozipokea mbio hizo za ainayake nchini.“Ninawashukuru ndugu zangu Watanzania kwa sababu bila ya ninyi kamwetusingefika hapa, asanteni kwa kuwaunga mkono wanariadha waliokimbiakwa umbali mrefu kutoka Dar es Salaam hadi hapa, na asanteni kwakuiunga mkono Bia ya Kilimanjaro…tunaahidi kuendelea kuwafanya makubwazaidi Watanzania…“Tunajivunia mlima mrefu kuliko yote Afrika na tunajivunia bia yetu yaKilimanjaro…hatuna budi kuungana kuvitangaza vivutio vyetu,”alisisitiza Kavishe huku akielezea umuhimu wa mbio hizo zilizopewajina la “Fikisha Tanzania Katika Hatua za Juu”.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment