TIMU YA TAIFA YA POOL TABLE YAENDA BONDENI!!

Mchezaji wa Timu ya taifa ya Pool Table na nahodha wa timu hiyo Ally Akber Akberal akijaandaa kupiga mpira wakati walipokuwa wakiagwa kwenda kwenye mashindano ya mchezo huo ncini Afrika ya kusini yanayoanza kesho.(Picha na Rajabu Mhamila Super D Mnyamwezi)
Wachezaji wa mchezo wa Poll Table kutoka Tanzania wanatarajiwa kuondoka kesho kuelekea Afrika Kusini kwa ajili ya mashindano ya mchezo huo yanayotarajiwa kuanza kesho hiyohiyo muda wa jioni kwa saa za Afrika Kusini.
Wakizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Meeda ulioko Sinza jijini Dar es salaam wachezaji hao wamesema wamejiandaa vyema na wako tayari kwa mapambano yao katika mashindano huko Afrika Kusini.
Wachezaji wanaotarajiwa kuondoka kesho asubuhi kwenda nchini humo kwa michezo hiyo ni FeLix Atanas, Omary Akida, Godfrey Muhando, Ally Akber Akberali na Six Muhamed, katika mkutano huo leo wote kwa pamoja walishika bendera ya taifa kama ishara katika kutetea taifa lao la Tanzania watakapokuwa katika michezo hiyo.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

1 comments:

  1. Sio poll kaka, ni pool table..

Post a Comment