STAILI HII YA WASANII WETU KUVUA NGUO MAJUKWAANI IMEKAAJE WADAU!!

Msanii Afande sele akiwajibika jukwaani.
Afande Sele (Seleman Msindi) ni mmoja wa wasanii wa muzki wa kizazi kipya wanaofanya vizuri sana kwenye gemu ya muziki wa bongo fleva kwa muda mrefu sasa, msanii huyu ametoa nyimbo nyingi zinazogusa mambo mengi kwenye jamii na zenye mafunzo ya kutosha kwa mashabiki wake.
Katika kujaribu kuiteka hadhira katika maonyesho wasanii wengi wamekuwa na mbinu mbalimbali wanazotumia vikiwemo vituko kama hiki ili kuvutia mashabiki wao katika maonyesho yao.
Hii inayoonekana hapa ni moja ya staili aliyoamua kuitumia msanii afande Sele wakati akiwa jukwaani katika uleule utaratibu wa kujaribu kuwavutia mashabiki wake ili aweze kukubalika zaidi katika kazi zake za muziki
Staili hii inatumiwa pia na wanamuziki kadhaa kutoka mataifa yaliyoendelea kama vile Marekani wakati wanamuziki kadhaa wa muziki wa Hiphop wanapokuwa jukwaani hufanya vituko mbalimbali lakini kwao hii haina tatizo kutokana na utamaduni wao uliowazi zaidi.
Inawezekana Afande Sele aliamua kuiga staili hii ili kuteka mawazo ya mashabiki wake wakati alipokuwa akiimba jukwaani, lakini je? utamaduni wetu ukoje jamani hapa nyumbani, mi naona Afande alipitiliza zaidi kutokana na utamaduni wetu lakini pia simlaumu kwani kwa kufanya hivyo ni dhahiri kuwa kuna baadhi ya mashabiki aliwafurahisha pia.
Mimi nadhani wasanii mnayo nafasi ya kubuni ama kuiga mbinu mbalimbali ambazo zinaweza kuwafanya mkatawala majukwaa na kufanya vyema kwenye maonyesho yenu bila kuvua nguo jamani hamuoni kwamba kufanya hivyo mtakuwa mnafanya kitu tofauti na utamaduni wetu mbona kuna wanamuziki kama akina Chamelione kutoka Uganda au Nameless kutoka Kenya na wengine wengi wamekuwa wakifanya vizuri sana kwenye maonyesho yao lakini sijawahi kuona wakivua nguo sana unaweza kuona amevua shati tu na hii huenda inatokana na hali ya joto ,katika jiji la Dar es salaam.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment