- Shindano la Uniqmodo limetokana na kawaida ya kutoa kiasi cha shillingi kati ya 50/100,000/= kwa mwezi kwa mamodo ambao kwa ridhaa yao, hutuma picha na maelezo yao kwenye blog yangu ili niwakuze miongoni mwa wadau wa maswala ya umodo. Ni faraja kuona kwamba wengi sasa wanapata kazi za umodo.
- Blog ya Umodo inakaribia kutimiza mwaka mmoja, nikaona ni vema niitishe shindano kubwa zaidi litakaloshirikisha mamodo wa kike kwa mwaka huu ili nitoe zawadi ya jumla ya miezi 12. Yaani 1,200.000/=.Hilo lilikuwa wazo langu hadi ambapo nilipojiunga na Gazeti jipya liitwalo Ok! Kila Wiki. Dau likaongezeka.
- Mfumo wa shindano nao ukabadilika, na sasa tutafanya usaili wa wasichana wengi iwezekanavyo kutoka wilaya 3 za Dar es salaam.
- Usaili utaanza tarehe 7 Novemba na tutachuja wasichana hadi wafikie 20 kila Wilaya na ndio hao watakaowakilisha wilaya.
Kigezo kikuu ni: UZURI HALISIA. Yaani NATURAL BEAUTY. Hatutajali sana ufupi, urefu, nk. Hii inatokana na "aina" ya wasichana waliopo nchini na pia Umodo kama unavyofahamu sio kupita jukwaani tu.
Kuelekea mwisho wa Mwezi Oktoba, naweza kuomba msaada wako zaidi na hata ushiriki ukiwa ni mdau mkuu wa maswala ya UREMBO.
1 comments:
Kaka,
AHSANTE SANA kwa kupost tangazo. Nimetuma kwa wengi lakini ni wachache wenu mlio na moyo wa kiuungwana.
Nisaidie kitu kimoja tu, nirekebishie kiasi cha fedha katika maelezo. Sio 100.00/= inatakiwa iwe Ths 100,000/= kuna sefuri inakosekana!
Nakushukuru mno!!!
Post a Comment