Katibu mkuu mpya Wizara ya Habari utamaduni na Michezo Bwana Sethi Kamuhanda akila kiapo mbele ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi katika hafla ambayo Rais aliwaapisha Makatibu wakuu wanne wapya pamoja na Mwanasheria mkuu na Naibu wake. (picha na freddy Maro)
Katibu wa Rais Mpya Bwana Prosper Mbena(kulia) akipongezana na katibu mkuu mpya wa wizara ya Nishati na Madini Bwana David Jairo(kushoto) muda mfupi baada ya hafla ya kuwaapisha iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.Kabla ya uteuzi mpya Bwana Jairo alikuwa Katibu wa Rais
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitaniana na Bertha Jairo(7) binti wa Katibu Mkuu Mpya wa Wizara ya Madini na Nishati Bwana David Jairo wakati wa hafla ya kuwaapisha makatibu wakuu wapya wa wizara mbalimbali zilizofanyika ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.Kabla ya uteuzi mpya Bwana Jairo alikuwa katibu wa Rais.
0 comments:
Post a Comment