Mkurugenzi wa Kampuni ya Kelken Tours & Safari, na Kelken Gym & Fitness, Genoveva Kiliba,zote za jijini,amejitokeza kusaidia shindano la miss Utalii Tanzania 2009-Temeke.akizungumza katik Ofisi za Kelken Fitness Gym, Genoveva Kiliba, alisema kuwa wameamua kusaidia shindano hilo ikiwa ni katika kukuza sanaa ya Urembo ambayo kwa sasa inazidi kukua hapa nchini."ni kweli kabisa kampuni yngu ya Kelken nikishirikiana na baba watoto wangu ambaye yeye ni mkurugenzi upande wa Kelken Tours & Safari, Payas Moremi, tutasaidia kufanikisha shindno la Miss Utalii Temeke ikiwa pia ni kutoa mchango wetu katika wilaya yetu ya Temeke ambako ndiko ofisi zetu za Fitness Zinapatikana, Udhamini tutakaowapa ni pamoja na kuwaweka gym Warembo hadi siku ya Onyesho pamoja na mengine" alisema Genovevaaidha kampunio hiyo ni ya pili kutangaza waziwazi kusaidia shindano hilo baada ya kampuni ya Ulinzi ya Aurora kujitokeza mwishoni mwa juma na kuhahidi kuwasaidia warembo ho katika badhi ya mahitaji muhimu ikiwa ni pamoja na kuwapatia Usafiri wa Ndani wakiwa jijini Dar es Salaam,Shindano la Miss Utalii Temeke litafayika katika tarehe 25 mwezi huu, ambapo jumla ya warembo 12 wanatazamiwa kupanda jukwaani kuchuana ikiwa ni maadalizi ya kwenda kushiriki katika Fainal za Miss Utalii Taifa zilizopangwa kufanyika hpo baadaye.
Naye mratibu wa Miss Utalii Tanzania 2009-Temeke, Linda Masanche alisema kuwa anawashukuru wote ambao mpaka sasa wametangaza kusaidia kufanikisha shindano hilo ambalo kwa mwaka huu ni la pili kufayika bada ya Kumalizika kwa Miss Utalii Vyuo Vikuu 2009-kanda ya Mashariki."ninashukuru kwa kweli kupata Udhamini huu wa wazi, ni jambo gumu kwa mtu kujitokeza kusaidia bila kupewa barua ya kuombwa, ukweli watu kama hawa ni wachache sana ambao inabidi wawe mfano wa kuigwa, ila ninawaomba watanzania hasa wenye uwezo watusaidie kufanikisha shindano hili mkwa upande wa Temeke"alisema Linda Masanche.jumla ya warembo 12 wanaendelea na mazoezi katika Ukumbi wa Cituy Gardeni Kariakoo Dar es Salaam chini ya walimu Rose William, ambaye pia ni miss utalii namba mbili Vyuo Vikuu 2008, na Miss Utalii Tanga 2008 Doreem Kesy.
0 comments:
Post a Comment