Burudani ya kundi maarufu hapa nchini kwa sasa THT ilitia fora pale walipoigiza baadhi ya nyimbo za Gwiji wa muziki wa Pop Duniani Marehemu Michael Jackson, vijana hao walicheza kwa umakini na umahiri mkubwa sana kitu kilichokuwa kigumu kuwatofautisha harakaharaka wasanii hao na gwiji huyo, lakini pia niseme kamati ya Miss Tanzania kupitia kwa majaji wao walifanya kazi nzuri kwani hakukusikika malalamiko yeyote kutoka kwa mashabiki waliofurika ukumbini hapo, mara baada ya kumalizikia kwa shindano hilo mbali ya watu kuondoka na wengine kushangilia kutokana na matokeo hayo hivyo wana wa FULLSHANGWE tunawapongeza wandaaji wa Miss Kinondoni kwa kazi kubwa waliyofanya mpaka kufanikisha shindano hilo katika viwango vya juu, wengine katika picha ni Yvonne Bigirwa mshindi wa pili na aliyeko kushoto na kulia ni Aloycia Innocent mshindi wa tatu.
REDDS MISS KINONDONI FUNIKA BOVU, MASHABIKI WASHIBA ZOMBO NA MATEMBELE!!
Posted by
ADMIN
You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment