Makamu wa Rais Zimbabwe Marehemu Joseph Wilfred Msika azikwa!!

Jeshi la Wananchi wa Zimbabwe likiwa limebeba jeneza lenye mwili wa Marehemu Joseph Msika(85) aliyekuwa Makamu wa Rais Wa zimbabwe tayari kwa maziko katika makamburi ya mashujaa wa Zimbabwe. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliiwakilisha serikali katika Maziko hayo yakiyofanyika jana.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Ali Mohamed Shein akimfariji Mjane wa Marehemu wa Makamu wa Rais wa Zimbabwe Mama Mai Maria Msika wakati alipomtembelea nyumabni kwake nje kidogo ya Mji wa Harare kutoa salamu za ploe kufuatia kifo cha Makamu wa Rais wa Zimbabwe Joseph Wilfred Msika. Katikati ni Mama Mwanamwema Shein.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Ali Mohamed Shein akitoa heshima za mwisho kwa Marehemu Joseph Wilfred Msika nyumbani kwake kabla ya maziko ambayo yamefanyika jana katika makaburi ya mashujaa wa Zimbabwe. Nyuma ni Mke wa Makamu wa Rais Mama Mwanamwema Shein. Dk Shein ameiwakilisha serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Maziko hayo.Picha? Clarence Nanyaro/VPO

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment