VIFAA VYA SIMBA SPORTS CLUB VYAANZA KUWASILI JIJINI TAYARI KUJIUNGA NA TIMU HIYO!!

Mchezaji wa kutumainiwa wa Timu ya Taifa ya Kenya (Harambee Stars) aliyejiunga na Simba Sports Club msimu huu wa 2009/2010 Hirary Echessa akiwa katika uzi mwekundu wa timu yake ya Simba mara baada ya kuwasili jijini leo akitokea nyumbani kwao Nairobi nchini Kenya kwa ajili ya kukipiga na timu yake mpya ya Simba.
Echessa amesema anajisikia furaha na amekuja kuifanyia simba mambo makubwa akishirikiana na wachezaji wenzake wa timu hiyo, Echessa ameongeza kuwa katika umoja kila kitu kinawezekana, na ana imani kubwa na Simba, wachezaji wa timu hiyo na kwamba anaamini kuwa atapata ushirikiano mkubwa kutoka kwa wachezaji wenzake, hivyo kuifanya simba ipate mafanikio makubwa msimu huu wa ligi kuu ya Vodacom inayotarajiwa kuanza mwezi Agosti na Mashindano ya kimataifa pia.
Kiungo mpya wa timu ya Simba na mchezaji wa kutumainiwa wa Harambee Stars raia Hirrary Echessa akiwa amjipumzisha katika mgahawa wa Hadees mara baada ya kuwasili leo akitokea nyumbani kwao nchini Kenya Mchezaji huyi amejiunga na simba kwa msimu huu wa 2009/2010

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

1 comments:

  1. naomba nirudie tena hii blog yako ndio maana aina watu wa kuchangia maoni kwasababu umezidi unazi sana weweee.. ni habari za simba tu ndio unaziona.. basi iite fullsimba...tuweelewe...sijawai kuona ata sikumoja umeandika habari za timu nyingine... badilika weweee... watu wengi wansoma blog nyingine lakini yako ni ya unaziiiiiiiiiiiii. ujumbe umekufikia......na hicho sio kifaaa bali na galasa hilo

Post a Comment