Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa amembeba mtoto Monde Muteka anayelelewa katika kijiji cha watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu cha (SOS) kilichopo katika mji wa Livingstone nchini Zambia . Mama Kikwete alitembelea katika kijiji hicho hivi karibuni ili kuona jinsi watoto hao wanavyolelewa kituoni hapo.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete (katikati) na Mke wa Rais wa Zambia Mama Thandiwe Banda (kulia) wakiangalia chumba wanacholala baadhi ya watoto wanaolelewa katika kijiji cha watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu cha (SOS) kilichopo katika mji wa Livingstone nchini Zambia . Kushoto ni Esther Balengu ambaye ni mama mlezi wa nyumba hiyo. Wake hao wa Marais walitembelea katika kijiji hicho hivi karibuni ili kuona jinsi watoto hao wanavyolelewa kituoni hapo.
Picha na Anna Nkinda - Maelezo
Picha na Anna Nkinda - Maelezo
0 comments:
Post a Comment