
John Momadi aka (John Tall) wa Mbezi Beach akimlisha mkewe Scolastica Massawe Keki kama ishara ya upendo mpaka kifo kitakapowatenganisha mara baada ya kufunga ndoa yao takatifu katika kanisa la Assembliese Of God kwa mama Mchungaji Dk Getrude Rwakatale jana jioni na kufuatiwa na hafla ya kupendeza iliyofanyika kwenye ukumbi wa Police Officers Mess Oysterbay jijini jana FULLSHANGWE ianwapa shavu sana bibi na bwana John Momadi Mungu awajalie na kuwazidishia katika maisha yenu mpate watoto wa kutosha ila! muwapige( the Nondooz za kutosha ) ili kila mmoja angalau awe na Shahada mbili za elimu ya juu nafikiri itakuwa bomba sana.

Hapa Bwana na Bini John Momadi wakijiandaa kukata keki tayari kwa ajili ya kulishana huku wasaidizi wao Bwana na Bini Evarist Hagila wakiwaangalia wakati wa sherehe iliyofanyika kwenye Bwalo la Polisi Oysterbay jana.

Bw. John Momadi maarufu kama (John Tall) wa Mbezi Beach na Bi. Scola Massawe wakitoka kanisani mara baada ya kufunga ndoa yao takatifu katika kanisa la Assemblise Of God lililoko Mikocheni, ama kama wanavyopenda kuliita watumishi wa mungu kwa mama Mchungaji Dk. Getrude Rwakatale jana jijoni na kufuatiwa na sherehe ya kukata na shoka pale katika Bwalo la Polisi Oysterbay jijini.
0 comments:
Post a Comment