Habari kutoka katika eneo la ajali Baharini inayoihusisha Meli ya MV Fathi huko visiwani Zanzibar, zinasema mpaka sasa ni maiti tatu zimeopolewa na majina yao bado hayajatambuliwa huku kazi ya kuokoa miili ambayo bado imekwama katika meli hiyo ya mizigo ikiendelea.
Meli hiyo ilikuwa ikijiandaa kwenda Dar es alaam kutoka Zanzibar ikiwa na shehena ya mizigo mbalimbali na watu kadhaa, haijajulikana mpaka sasa ni watu wangapi wako ndani ya meli hiyo wakiwa hai, na ni wangapi wamekufa, bado tunaendelea kusubiri taarifa za vyombo vya usalama ili kujua sababu za kutokea kwa ajali hiyo na idadi ya watu waliokufa au kuokolewa pamoja na hasara ya mali, mara tutakapopata taarifa zaidi tutawaleteeni mara moja.
0 comments:
Post a Comment