Mwenyekiti wa kijiji cha Nyamatongo Wilayani Senerema mkoani Mwanza Bw. Samwel Kwangelija akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya Habari maelezo juu ya manyanyaso na uporwaji wa ardhi yao ekari zipatazo arobaini inayodaiwa kuporwa na anayedaiwa kuwa Mwekezaji raia wa Uganada Bwana Shaban Ally mkazi wa mwanza mjini.
Bwana Kwangelija ameongozana na baadhi ya wazee wa kijiji hicho wanaodai kushitakiwa na mfanyabiashara huyo juu ya suala la kumiliki ardhi hiyo kama unavyowaona katika picha Matius Shibungi wapili kutoka kulia Kayenze Mapuri na Joseph Madiro.
Mwenyekiti huyo ameonyesha baadhi ya vielelezo kwa wanahabari ambavyo vinaonyesha kuwa ameshapeleka malalamiko ya wanakijiji hao katika ngazi zote ikiwemo ofisi ya halmaghauri ya Wilaya ya Sengerema, Ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mwanza na katika mahakama ya Rufaa, pia amefika Dodoma na kumuona Mbunge wa Jimbo hilo Mh. William Ngereja na Ofisi ya Waziri Mkuu mbapo mwenyekiti huyo wa kijiji cha Nyamatongo amedai hakupata ushirikiano.
0 comments:
Post a Comment