Kijana huyu si mwingine ni Francis Casto kutoka Mbeya amabaye ni miongoni mwa washindi watatu waliopatikana katika shindano la Vodacom Global Soccer Star, wenzake ni Salum Saad kutoka Zanzibar na Cosmas Mwazembe kutoka Mbeya.
Rwehumbiza amesema Fracis Casto anaenda nchini Ubeligiji katika shule maalum ya soka inayoitwa Cecle Brugge na atakuwa nchini humo kwa muda wa wiki mbili akifanya majaribio hayo, Casto ataondoka leo usiku na ndege ya shirika la ndege la KLM wakati washindi wengine wawili Saad na Mwazembe wakisubiri mipango yao ya kwenda kufanya majaribio ikikamilishwa, katika picha wengine ni Francis Casto kulia na Emillian Rwejuna meneja udhamini Vodacom.
0 comments:
Post a Comment